Mambo Muhimu Ya Kuwa Na Hadhari Nayo
Mtu akifariki na kwa bahati mbaya hana jamaa wa kumsimamia kuzikwa kwake na hakuwahi kujiunga na aina yoyote ya mfuko Borough/city council itachukua jukumu hilo
Mara nyingi huzika kwa kuuchoma moto mwili wa marehemu ili kupunguza gharama
Taratibu za kiislamu hazitofuatwa
Waislamu watakuwa na dhimma kwa kushindwa kutekeleza jukumu lao la Fardhi
Gharama za mazishi zinabaki kuwa deni lenye kuongezeka kwa riba (interest) kama halijalipwa kwa muda uliowekwa
Uchunguzi wa maiti unaweza kupendekezwa na madaktari kujua sababu ya kifo lakini itakuwa bora zaidi kama hautofanyika kwani utachelewesha taratibu za mazishi na Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amependekeza kuharakishwa kwa maziko.