Al-Iman Society of Northamptonshire

Login   |    Signup  |

Madrasah - Utambulisho

Madrasatul Iman al – Islamiyyah ni madarasah ya wanafunzi wa kiislamu wanaotoka Afrika ya Mashariki na kwa sasa wanaishi Northampton na vitongoji vyake hapa Uingereza.

Wakaazi wa Northampton wanaotoka Afrika ya Mashariki ambao walianza kuhamia mji huu kwa wingi kuanzia mwaka 1998 waliona haja ya kuwa na madrasah ya kuwasomesha watoto Quraan na mafundisho ya dini . Na jitihada hizi hatimae zilizaa matunda na kufanikiwa kufungua madrassah kwa kushirikiana na ndugu zetu wa kiislamu kwenye msikiti wa Markazi Masjid uliopo 112-116 Abington Avenue Northampton hapo September 2003

 

Madrasah ilipoanza ilikuwa na wanafunzi 35 wanaume 20 na wanawake 15. Na walimu walikuwa 6 wanaume watatu na wa kike watatu. Na kufikia July 2005 kuna wanafunzi 90 wanaume 50 na wanawake ni 40. Maustaadh ni 10 wa kiume ni sita na wa kike wane ambae wamejitolea katika amali hii ya kheri.

Mwaka  2012 Madrasah ina jumla ya wanafunzi 310 wakiume 170 na wa kike 140 na jumla ya walimu 28

 

Hali kadhalika kumeundwa kamati ya wazazi ambayo kazi yake ni kuisimamia na kuwa kiungo kati ya uongozi wa Madrassah, Msikiti na Wazazi. Kamati hii ina Mwenyekiti, Katibu na wajumbe wawili ambao huchaguliwa kila mwaka.

Madrasah kwa sasa ina wanafunzi wenye asili ya Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Rwanda, Algeria, Sudan  na Uingereza na siku za masomo ni Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 8.30 mchana. Vijana wakubwa wa kiume kuanzia sa 1:00 Asubuhi mpaka saa 4.