Makosa Ndani Ya Swalah (1) | Al-Iman Official
Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy

Sep 2, 2018

Makosa Ndani Ya Swalah (1)

0 comments

 

Imekusanywa na Muhammad Faraj As-Sa’ay

Utulivu (Tumaaniynah)

 

Utulivu (Tumaaniynah) ni nguzo muhimu sana katika nguzo za Swalah, na bila ya utulivu Swalah haiwi kamilifu.

Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa amekaa Msikitini, akaingia mtu mmoja na kuswali. Baada ya kumaliza akainuka na kwenda kumsalimia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamuambia:

“Rudi kaswali tena, wewe bado hujaswali.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alimrudisha mtu huyo mara tatu, na kila anapomaliza kuswali alikuwa akimuambia:

“Rudi kaswali tena, wewe bado hujaswali”.

Yule mtu akamuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam):

“Sijui kuswali vizuri kuliko hivi, (bora) nifundishe”.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamuambia:

“Unapotaka kuswali tia udhu, kisha elekea kibla, kisha soma utakachoweza kusoma katika Qur-aan, kisha rukuu mpaka utulie (Tumaaniynah) na uwe na uhakika kuwa umerukuu (sawa), kisha inuka usimame sawa sawa (Tumaaniynah), kisha usujudu mpaka utulie (Tumaaniynah) na uwe na uhakika kuwa umesujudu sawa, kisha kaa vizuri mpaka utulie katika kikao chako (Tumaaniynah), kisha sujudu na utulie (Tumaaniynah) mpaka uwe na uhakika kuwa umesujudu sawa, kisha ufanye hivyo hivyo mpaka umalize kuswali”Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah

 

 

 

Hadiyth hii na nyingi kama hizi zinatujulisha kuwa Swalah haiwi kamili bila ya utulivu (Tumaaniynah). Nako ni kutulia katika kila kitendo cha Swalah. Mtu anatakiwa atulie mpaka awe na uhakika kuwa ametulia.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amempa jina la ‘Mwizi’ mtu anayeswali bila utulivu.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

“Katika wezi wabaya kabisa ni wale wanaoiba katika Swalah zao, hawarukuu kwa ukamilifu wala hawasujudu kwa ukamilifu na hawawi na khushuu.”

 

 

 

Na katika riwaya nyingine amesema juu ya ‘Mwizi wa Swalah’:

 

“Na wala haunyoshi mgongo wake sawa pale anaporukuu na anaposujudu.”

 

Imaam Ahmad, Al-Haakim na imesahihishwa na Imaam Adh-Dhahabiy.

 

 

 

 

 

Kudokoa

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza kudokoadokoa katika Swalah. Kwa sababu anayeswali kwa pupa bila ya utulivu anakuwa mfano wa kuku anayedokoa mtama, na huwa haipi haki yake Swalah, wala hakipi kila kitendo haki yake. Bali hampi Mola wake haki Yake.

 

Kumbuka kuwa ndani ya Swalah yanapita mazungumzo baina yako na Mola wako (Subhaanahu wa Ta’ala).

 

 

 

Katika Hadiyth ambayo sehemu ya mwanzo yake ni Hadiyth Al-Qudsiy, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

“Mwenyezi Mungu Anasema; ‘Nimeigawa Swalah baina yangu na baina ya mja wangu sehemu mbili, na mja wangu (ninampa) anachoniomba’. Mja anaposema:

 

 

 

 

 

"الشوق للوهو ربوو الجلالومينو" MwenyeMungu Husema: “Mja wangu amenishukuru”

 

 

Na anaposema:

 

 

"الرومنسم الرومى" ،

Mwenyezi Mungu Husema: “Mja wangu amenipa sifa yangu”.

 

 

 

Na anaposema:

 

مَلَهُو يَوْمُو الدُّنُو”,

 

Mwenyezi Mungu Husema:

 

“Mja wangu amenitukuza”, au Husema:“Mja wangu amejisalimisha kwangu ”.

 

 

 

Na anaposema;

 

يوريوآكَ نَتَبُ وُيَيَاوَكَ نَوْرَوِنِي”,

 

Mwenyezi Mungu Husema:

“Haya ni baina yangu na baina ya mja wangu na mja wangu atapata atakachoniomba.”

 

Na anaposema:

اهنؤوا الزورواتا المعزوفيمو. زهورهم الُنَوَنَ أَلْنَوَوَ فَلِيَوْمُ شَيْئُو الْمُضَغِّلُ فَلْيُوْمُوْم وَلَا الأَوَاوِيُّ

”.

Mwenyezi Mungu Husema:

“Hii ni ya mja wangu na mja wangu atapata anachoniomba”

 

Mtu anapozungumza na mzee wake au mkubwa wake wa kazini au anapozungumza na mfalme katika wafalme wa dunia, huzungumza naye kwa heshima na utulivu kubwa.

 

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) Anastahiki zaidi heshima na utulivu huo kuliko viumbe hao dhaifu.

 

Mmoja katika Maulamaa amemfananisha anayeswali kwa pupa bila ya utulivu kuwa ni sawa na mwenye kunywa dawa chungu anapoweka chungwa lake tayari apate kula mara baada ya kunywa dawa kwa ajili ya kuuondoa uchungu wa dawa. Lakini yule anayestarehe ndani ya Swalah yake, mfano wake ni mfano wa mtu anayekunywa kinywaji kitamu. Anakunywa taratibu, akistarehe nayo huku akitamani kinywaji hicho kisimalizike.

 

Mtu anapomjua Mola wake, na kuzijua neema alizopewa, kisha akaujuwa uwezo wa Mola wake juu yake, huyo ndiye anayemjua Nani anayemuabudu, na anampa heshima anayostahiki.

 

Ibn al-Qayyim amepiga mfano wa mtu anayemuabudu Mola wake bila ya kumpa heshima anayostahiki kuwa ni mfano wa panya aliyemuua ngamia, kisha akamchukua ngamia huyo na kumpeleka penye tundu lake (tundu la panya) na kumtaka mkewe (ngamia) aingie ndani humo.

 

Ngamia akamwambia panya:

“Sikiliza bwana, nitafutie nyumba kiasi changu, au tafuta mke kiasi chako”

 

ibn al-Qayyim alimaliza kwa kusema:

“Na hivi ndivyo ilivyo, mtu ama amuabudu Mwenyezi Mungu kama Anavyostahiki kuabudiwa, au atafute kijiungu chake akiabudu kama anavyotaka yeye.”