Vinavyohitajika Unga wa ngano kilo 1 Hamira vijiko 2 vya kulia chakula Chumvi Ufuta Siagi ¼ kilo Samli aina yoyote vijiko 2 vya kulia chakula Mayai 5 Maziwa magi 1 Namna ya kutayarisha na kupika · Changanya unga kwa kutia maziwa, siagi, mayai, chumvi na hamira. · Ili ukandike vizuri unaweza kuongeza maji. · Unga ukishakandika, weka samli na uukande kidogo. · Kata madonge kwa shepu uipendayo au tumia vibati vya kuchomea mikate. · Weka ufuta juu yake na uwache uumuke vizuri. · Choma kwenye oven kwa gas mark 5 au umeme 250 · Baada ya dakika 10 itakuwa tayari ishawiva, lakini pia inategemea nguvu ya oven. Kidokezo · Ni mizuri kwa chai ya maziwa au ya rangi (chai kavu)