Vinavyohitajika Mchele vikombe 3 Kuku mgumu 1 Thomu/tangawizi ya kusaga vijiko 3 Mdalasini wa unga vijiko 2 vya chakula Kotmiri kishada kimoja Mbatata 4 kubwa Zabibu kavu Vitunguu maji 10 vikubwa Bizari nzima vijiko 4 vikubwa (uzile) Chumvi kiasi Mafuta ya kupikia Magi vipande viwili Namna kutayarisha na kupika · Teleka kuku na umtie chumvi pamoja na mchanganyiko wa thomu na tangawizi na mdalasini muache awive lakini umbakishe na supu kiasi ya magi 1. · Chambua majani ya kotmiri uyaoshe na uweke pembeni. · Kaanga vitunguu maji viwe rangi ya zaafarani (golden brown). · Menya mbatata na uzikaange ziwe rangi ya zaafarani(zikate vipande vidogo vya kiasi) Namna ya kutayarisha wali na kuchanganya · Roweka mchele kwa maji ya baridi kwa dakika 5 · Teleka sufuria ya maji ya wali na utie uzile uchemkie pamoja · Uzile ukisha toa rangi, utowe kwa kichujio cha chai na weka mchele uchemke mpaka ukiukata uwive kiasi (ukiubinya kwenye mwiko ukatike. · Uchuje wali maji na tayari kuuchanganya. · Weka mafuta uliyokaangia vitunguu kwenye sufuria kiasi kijiko 1 cha kula · Weka wali robo chini ukifuatiwa na kuku na supu yake kiasi. · Tandaza kotmiri nuru zabibu kiasi na funik a kwa vitunguu vyako ulovikaanga nusu ·Endelea kutia wali wako na kuufuata mfumo huo huo na ukimaliza kwa mbatata na vitunguu ·Malizia kwa kuufunika kwa wali uliobakia na nyunyiza vijiko 3 vya mafuta uliyokaangia vitunguu. · Funika foil na mfuniko ili mvuke usitoke na uweke kwenye moto mdogo mdogo uwive vizuri kwa dakika 45. · Ukipendelea kutia kwenye oven pia utawiva vizuri tu. Kidokezo Ni wali wenye ladha nzuri na harufu ya kuvutia ukiupatia saladi na ndizi mbivu unapendeza zaidi.