Zioshe mboga mboga za kachumbari kwa maji ya vuguvugu
Zikatekate zote kwa pamoja na uziweke kwenye mashine ya kusagia (Food Processor)
Isipokuwa ndimu tu ndio utakuja kuiweka mwisho
Zisage kwa kutumia numbari mbili kwa kusita kwa kila sekunde 1 mpaka kachumbari ichanganyike vizuri.
Ikishanganyika, weka maji ya ndimu na itie kwenye bakuli tayari kwa kuliwa.
Kidokezo
Pendelea kuosha mboga mboga za saladi kwa kutumia maji ya moto (lakini si ya kuwivisha) ili kuuwa vijidudu. Pia usisage kwa muda mrefu ili kuepuka kuwa na maji mengi.