Vinavyohitajika Siagi 250g Sukari 250g Arki rose kijiko 1 cha chai Zabibu 100g Unga wa ngano 100g Mayai 6 Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Namna ya kutayarisha na kupika Changanya siagi na sukari mpaka ichanganyike vizuri. Weka mayai kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari. Tia arki. Changanya unga na baking powder. Utie unga kwenye mchanganyiko wa mayai, siagi sukari kidogo kidogo mpaka uone haukushiki mikononi. Ipake siagi au mafuta sahani ya kuokea - tray na uzipange rock cake. Zichome kwa gas mark 5 mpaka ziwe na wekundu wa kupendeza. Kidokezo Jitahidi zisikauke na zikaungua sana zitakuwa ngumu na kila zikikaa zinazidi kuwa nzuri.