Vinavyohitajika Cheese (Jibini) 250g Delicate dill (ni aina ya majani ambayo huleta harufu nzuri kwenye chakula kama ilivyo nanaa na kotmiri. angalia kwenye picha) Mayai 5 Unga wa ngano magi 4 Chumvi Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Single cream au double cream 300ml Siagi 250g Namna ya kutayarisha na kupika Changanya unga, siagi na baking powder pamoja na chumvi. Kata kata delicate dill uchanganye kwenye unga. Ikate Jibini kwenye chombo cha kukatia - Grater na kisha itie kwenye unga. Yachanganye mayai na cream uyachape vizuri. Anza kumimina mchanganyiko wa cream na mayai kwenye mchanganyiko wa unga. Utapata mchanganyiko uliokuwa laini lakini unaweza kusukumika. Weka unga mkavu kwenye kibao cha kukatia usukume na kata shepu uipendayo. Zipange kwenye tray ya kuchomea. Paka yai juu ya scones. Zichome kwa muda wa dakika 25 to 30 kwa gas mark 5. Zikiwiva ziache zipoe na tayari kwa kuliwa. Kidokezo Scones unaweza kuzifanya kwa shepu uipendayo, hasa watoto ni chakula wanachokipenda na ni kizuri kwa afya yao kwa sababu ya jibini. Pia kwa kupata rangi nzuri ya kupendeza paka yai lilochanganywa na double au single cream