KUNUIA HAJJ NA UMRA
Labbayka Allahumma UmraNimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Umra Labbayka Allahumma HajjNimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Hajj
TALBIYAH
Labbayka-Llaahumma labbayk labbayka laa shariyka laka labbayk inna-l hamda wa-n ni'mata laka wa-l mulk, laa shariyka lak Tumeitikia Ewe Mola tumeitikia, Tumeitikia kwani huna Mshirika Tumeitikia, Hakika Himdi (shukurani) na Neema zote ni zako na Ufalme ni wako na huna mshirika.
KUINGIA MSIKITINI
Allaahumma salli `alaa muhammadin wa sallim, allaahumma aftah lee abwaaba rahmatika. Allah, Msalie muhammad na umfikishie salamu, O Allah nifungulie milango ya rehma zako..
KATI YA KONA YA YAMANI NA JIWE JEUSI
Rabbanaa aatinaa fi-d dunyaa hasanatan wa fi-l aakhirati hasanatan wa qinaa 'adhaaba-n naar. Allah tunakuomba utupe yenye kheri katika dunia na yenye kheri akhera na utuepushe na adhabu ya moto.
KUNYWA MAJI YA ZAMZAM
Ibni Abdallah ibn Abbas alikuwa akiomba kwa kusemaAllahumma inni as’aluka I’lman naafian wa rizkan waasian wa shifa’an min kulli daainO’ Allah ninakuomba elimu yenye manufaa na riziki yenye kujitosheleza na shifaa kutokana na kila maradhi.
SAFA NA MARWA
Inna-s safaa wa-l marwata min sha'aa'iri-l llaahi faman hajja-l baita aw i`tamara falaa junaaha 'alaihi an yattawwafa bihimaa wa man tatawwa'a khairan fa inna-l llaaha shaakirun 'aleem. Hakika vilima vya Safa na Marwa ni katika alama za Allaah. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Allaah ni Mwenye shukrani na Mjuzi.”
ARAFAT
"Laa ilaha illallaahu wahdahu laa shareeka lahu lahul mulk wa lahul hamdu wa huwa 'alaa kulli shay'in qadeer.” Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hana mshirika, Ufalme wote ni wakeZ na himidi ( shukurani) zote ni kwake naye ni muweza wa kila jambo.