Kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Na Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam) | Swahili | Al-Iman Official
Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy

Aug 4, 2018

Kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Na Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam)

0 comments

Imetayarishwa na Shani Ahmad Namshukuru Mwenyezi Mungu, ambae Ametuumba na Akatuweka katika ulimwengu ili tumuabudu Yeye pekee. Na Akatupa miongozo yenye kutuwezesha kuishi katika huu ulimwengu Aliotuumbia. Kisha Akatuletea wajumbe ili watufunze na kutubainishia miongozo hiyo ili tupate kuongoka. Napenda kuchukua nafasi hii, pia nakuomba na wewe msomaji kuchukua nafasi hii kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), mbashiri wetu na muonyaji wetu. Kisha ningependa kuanza kwa kusema; Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipotuumba akatuweka katika huu ulimwengu hakutuwacha tuu, bali alituwekea miongozo ambayo itaweza kutufikisha katika mafanikio ya upeo wa ubora wa maisha duniani. Akatuletea Mitume ili waje kutufunza na kutuongoza, Akawapa vitabu na sahifa zilizojaa uongofu na rehema Zake. Ili tupate mafanikio hapa duniani ni lazima tufuate miongozo hii itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tuwafuate Mitume salawatu Llaahi wasalaamuhu ‘alayhim. Amesema Mwenyezi Mungu:

“Na watahadhari wale wanaopinga amri zake (Mtume) itawapata fitnah au itawapata adhabu iumizayo.” [An-Nuur 24: 63]
Amesema Ibn ‘Uthaymiyn katika Uswuul min ‘Ilmil-Uswuul, ‘kutokana na aya hii tunapata dalili ya kuwajibika twaa ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kwa vile Mwenyezi Mungu Anawahadharisha wale wanaopinga amri za Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa itawapata fitnah ambayo ni misukusuko katika maisha ya dunia au adhabu iumizayo huko Akhera.

Maonyo kama haya hayaji ila kwa kuacha jambo la Wajibu, yaani ni kwamba amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pekee ni Wajibu kuitekeleza’. Endapo mwanaadamu ataacha kumtii Mwenyezi Mungu atakuwa ameacha kutekeleza Wajibu wake, hali ya kuwa amepinga amri ya Mola wake ya kumtii, hali hiyo itampelekea; Kwanza, kuingia katika dhambi ya uasi, ambayo Mwenyezi Mungu Ametuonya kwa adhabu kali ya moto kama Alivyosema katika Surat An-Nisaa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا - 4:59
“Enyi Mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wale wenye amri miongoni mwenu, na mtakapokhitilafiana juu ya jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa nyinyi ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho…” [An-Nisaa 4: 59]

Aya hii imetuwekea ubainifu kwamba yule ambae hatorudisha khitilafu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume basi huyo si katika Waumini. Hali kadhaalika tunapata mafunzo kama haya katika Surat An-Nisaa:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا - 4:65
“Si hivyo, naapa kwa mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe kuwa ndie hakimu juu ya yale yanayotokea miongoni mwao, kisha wasipate katika nafsi zao kipingamizi juu ya yale uliyohukumu na wajisalimishe kikamilifu.” [An-Nisaa 4: 65]

Haya ni mafunzo kutoka Mola muumba yaliyo wazi yasiyo na shaka, yenye kututhibitishia kuwa twaa ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio mhimili mkuu wa iymaan zetu na Uislam wetu mafunzo haya ni ubainifu ulio dhaahir kuwa bila ya twaa iymaan zetu na kujisalimisha kwetu ni bure na vipi utakuwa Muislam yaani mwenye kujisalimisha ikiwa bado hutekelezi amri za yule unayedai kuwa umejisalimisha kwake? Tatu, kutokufanikiwa katika yale anayokusudia kuyafanya kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu katika Suurat Twaahaa:

قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ - 20:123
”Akasema tokeni humo nyote, (kutakuwa na) uadui miongoni mwenu, na ama pale utakapokufikieni kutoka kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu wangu huo, basi huyo hatapotea wala hatotaabika.” [Twaahaa 20 : 123]

Katika aya hii kuna mazingatio makubwa, Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kuwa hata baba yetu Nabii Aadam na mama yetu Hawwaa walipokiuka mipaka yake na kuacha twaa Yake, Aliwatoa katika pepo, pamoja na kuwa walitubu. Aya imeendelea na kutufunza kuwa tutakapokubali kufuata miongozo ya Mwenyezi Mungu hatutopotea wala hatutotaabika. Na mwenye kupuuza amri za Mwenyezi Mungu basi huyo atapata maisha dhiki na taabu hata kama atakuwa na utajiri wa mali na watoto, kwa kutotii amri za Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) mali yake na watoto wake watamtia katika dhiki ameahidi hivyo Mwenyezi Mungu katika Surat Twaahaa kwa kusema:

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ - 3:132
“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.” [Aali ‘Imraan 3: 132]

Katika mafunzo ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni kwamba hatoingia peponi ila yule aliepata Rehma za Mwenyezi Mungu, hivyo tukumbuke kuwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni jambo kubwa mno kwetu, ila kwa yule asie taka pepo katika maisha yake ya Akhera. Na katika kumtii Mwenyezi Mungu tunapata Uongofu kama Alivyosema katika Suuratun Nuur: 54:

“na mkimtii mtaongoka”

Na katika faida za kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kupata utukufu wa kufufuliwa pamoja na watu wema waliohakikishiwa neema za Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, Masadiki, Mashahidi na Maswaalih. Kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Suurat An-Nisaa:

تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ - 4:13
وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ - 4:14
“Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Yeye (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza katika Bustani zipitazo mito mbele yake; wakae humo milele. Na huko ndiko kufaulu kukubwa.”
“na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kuiruka mipaka Yake, (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza Motoni, humo atakaa milele na atapata adhabu zifedheheshazo.” [An-Nisaa 4: 13-14]

Ndugu zangu faida nyingi na hatuwezi kuzidhibiti zote katika makala hii, ni juu yetu kuzijua hivyo tufanye jitihada kuzitafuta ikiwa ni moja ya kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ya kutafuta elimu. Inatupasa tukumbuke kuwa sisi ni Waislam na maana ya kuwa Muislam ni kujisalimisha au kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala), na kuyakubali yale yote aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kama ilivyopokelewa katika vitabu mbali mbali, amesema Abu Ja’afar At-Twahaawiy, katika ‘Aqiidat At-Twahaawiyyah, ‘Aqiydah namba 36,

“Na Uislam wa mtu hautathibiti pasi na kujisalimisha na kujiweka chini ya nguvu za Mwenyezi Mungu...”

Na kujisalimisha maana yake ni kuwa chini ya twaa ya Mwenyezi Mungu, kufanya kila Alilotuamrisha na kuwacha kila Alilotukataza, kumkusudia yeye tu katika ibada na mambo yetu yote ya maisha yetu. Ikiwa hatuwezi kuitimiza ahadi hii adhimu tuliyompa Mwenyezi Mungu ya kujisalimisha Kwake au kuwa tayari kutekeleza maamrisho Yake yote na kuyakubali yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) wapi tunashika katika kujivunia Uislam wetu? Maana Ya Sunnah Ni ufahamu wa wengi miongoni mwetu kuwa Sunnah ni vitendo au ibada ambazo tunapozitekeleza tunapata ujira, na tunapo yawacha hatutopata adhabu bali tutakosa ujira tu. Kutokana na ufahamu huu watu wengi wamejengeka na tabia ya kutotekeleza Sunnah na kusema ‘hiyo ni Sunnah tu si wajibu’, pale wanapotakiwa kutekeleza amri kati ya maamrisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kwa hakika Sunnah ni mafundisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), ikiwa ni miongoni mwa maneno, vitendo au yale yaliyofanywa mbele yake nae akayakiri. Na juu ya haya ndipo tunalazimika kutekeleza Sunnah katika hali ya kuwajibika juu yetu kama ilivyobainishwa katika aya zilizokwisha tangulia hapo juu. Aya ambazo zinatuhimiza kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Hali hiyo ya kuwajibika kwetu katika Sunnah inaondoka pale tu Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) anapotubainishia, au kubainishwa na wanavyuoni kwa kufuata taratibu zake zinazokubalika. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Fiqh Kwanza kabisa tufahamu kuwa Sunnah ni neno la Kiarabu lenye maana ya njia ‘mwenendo’ yaani ni jambo ambalo limetokea kisha watu wakafuata mwenendo au jambo hilo. Kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam):

“Mwenye kuweka mwenendo mzuri basi atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakaofuata mwenendo huo, na mwenye kuweka mwenendo mbaya atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakao fuata mwenendo huo...”

Hii ni maana ya Sunnah katika lugha. Ama katika matumizi ya Sunnah kwa wataalamu wa Fiqh, ni amali zilizo chini ya Waajib, zinakusanya kila kile ambacho Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekipendekeza ambacho hakiwajibiki kukifanya. Sunnah kwa mtazamo huu hujulikana kama Manduub (mapendekezo) na hupata ujira mwenye kuzitekeleza na hatoingia makosani yule mwenye kuziacha. (M. H. Kamali, Hadith Studies) Na huu ndio mtazamo ambao wengi wetu tunaufahamu, mtazamo wa ki- Fiqh ambao umelenga katika kutoa hukumu za kishari’ah, na si maisha ya Wanaadamu ya kila siku kwa ujumla. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Hadiyth Vivile katika historia ya Dini, neno Sunnah limetumika kwa namna kadha, kwa mfano Wanachuoni wa Ahlul-Hadiyth, wanaitambua Sunnah ni chochote kile kilicho thubutu kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Semi zake , Matendo yake, Yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia, historia yake, Tabia na Maumbile yake. Baadhi ya Maulamaa wamewaita Wanachuoni wa Hadiyth ndio Ahlu-Sunnah. Baadhi ya Wanachuoni wakubwa wa karne ya tatu Hijriyyah waliandika vitabu kuhusiana na ‘Aqiydah na kuyapa majina As-Sunnah. Zama hizo watu walikuwa wanajulikana ni watu wa Sunnah kama ni katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah. Pia ilitumika kinyume cha Sunnah; Bid'ah (Uzushi) kwa kubainisha wale ambao si katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Uswuuliyyuun Amma Wanachuoni wa Uswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika. serifUswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika.

New Posts
  • KUNUIA HAJJ NA UMRA Labbayka Allahumma Umra Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Umra Labbayka Allahumma Hajj Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Hajj TALBIYAH Labbayka-Llaahumma labbayk labbayka laa shariyka laka labbayk inna-l hamda wa-n ni'mata laka wa-l mulk, laa shariyka lak Tumeitikia Ewe Mola tumeitikia, Tumeitikia kwani huna Mshirika Tumeitikia, Hakika Himdi (shukurani) na Neema zote ni zako na Ufalme ni wako na huna mshirika. KUINGIA MSIKITINI Allaahumma salli `alaa muhammadin wa sallim, allaahumma aftah lee abwaaba rahmatika. Allah, Msalie muhammad na umfikishie salamu, O Allah nifungulie milango ya rehma zako.. KATI YA KONA YA YAMANI NA JIWE JEUSI Rabbanaa aatinaa fi-d dunyaa hasanatan wa fi-l aakhirati hasanatan wa qinaa 'adhaaba-n naar. Allah tunakuomba utupe yenye kheri katika dunia na yenye kheri akhera na utuepushe na adhabu ya moto. KUNYWA MAJI YA ZAMZAM Ibni Abdallah ibn Abbas alikuwa akiomba kwa kusema Allahumma inni as’aluka I’lman naafian wa rizkan waasian wa shifa’an min kulli daain O’ Allah ninakuomba elimu yenye manufaa na riziki yenye kujitosheleza na shifaa kutokana na kila maradhi. SAFA NA MARWA Inna-s safaa wa-l marwata min sha'aa'iri-l llaahi faman hajja-l baita aw i`tamara falaa junaaha 'alaihi an yattawwafa bihimaa wa man tatawwa'a khairan fa inna-l llaaha shaakirun 'aleem. Hakika vilima vya Safa na Marwa ni katika alama za Allaah. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Allaah ni Mwenye shukrani na Mjuzi.” ARAFAT "Laa ilaha illallaahu wahdahu laa shareeka lahu lahul mulk wa lahul hamdu wa huwa 'alaa kulli shay'in qadeer.” Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hana mshirika, Ufalme wote ni wakeZ na himidi ( shukurani) zote ni kwake naye ni muweza wa kila jambo.
  • Ummu Nasra  Kuna mambo mengi ya wazi kabisa ambayo sheria yameyakataza katika Uislamu na jamii imeghafilika nayo.  Mambo hayo huchangia  kuharibika na kuhatarisha mfumo  mzima wa kiislam ndani ya majumba. Miongoni mwa yenye kuhatarisha ni haya yafuatayo: 1. TELEVISHENI (TV) - LUNINGA. Televisheni kama inavyojuilikana (TV) ni chombo ambacho hakikosekani katika kila nyumba.  Kama kitatumika vizuri chombo hicho kwa mambo ya kheri yenye kuzidisha imani, kupeleka dini mbele, kukuweka mbali na maasi na kuhifadhi dini ya mja kinaweza kuleta faida.  Na kama kitatumika vibaya kinaweza kuathiri familia kwa asilimia kubwa kabisa.Ukweli ni kuwa kuangalia TV kuna madhara mengi na makubwa kuliko faida. Familia za kiislam zinaogelea kwa kasi kubwa bila ya kujali au kuona mabaya ya chombo hicho. Tuchukue mfano mdogo tu wa athari za televisheni kwa watoto kama utafiti huu mdogo uliofanyika hapa Uingereza unavyofafanua. Watoto wenye kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mawili kila siku wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa athma. Uchunguzi huo umeonyesha kuwa, kuangalia televisheni kwa muda mrefu kunaleta uwezekano wa kupata athma uongezeke mara mbili kwa watoto. Jinsi mfumo wa kupumua unavyofanya kazi wakati mtoto anapokaa tu bila kufanya chochote, hupelekea kutokea mabadiliko katika mapafu pamoja na magojwa mengine ya kupumua ikiwemo athma. Unene wa kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi kunakosababishwa na kuangalia muda mrefu televisheni hupelekwa kutokea hali hiyo Wataalamu wamesema kuwa, kuishi maisha ya kutokuwa na harakati yoyote katika umri mdogo hupelekea kuongezeka uwezekano wa hatari ya kupata athma ukubwani.Hivyo wamewashauri wazazi kuwashajiisha watoto wao kufuata maisha ya kawaida ya kuwa na mishughuliko na kupunguza muda wanaoutumia kuangalia TV. Wataalamu wa Uingereza wametoa taarifa hiyo baada ya kuwafanyia uchunguzi watoto 3,000  kuanzia wale waliozaliwa mpaka walio na miaka 11. Hasara moja ya kupoteza muda kuangalia TV inaweza kuzaa makosa mengi ndani yake.  Kuona na kusikiliza kuna wavutia wengi na kuwafanya watu kutawaliwa na tabia hiyo na kutoweza kuiepuka. Hakuna shaka kuwa jamii hasa watoto imeathirika sana na jambo hili.  TV inasababisha kwa kiasi kikubwa watoto wa Kiislamu kutumbukia katika tabia zisizo na maadili, ulevi, uzinzi, kukosa heshima, kujinasibisha na uzungu na mengi mengine maovu tunayoyaona katika jamii zetu.  Yote hayo wanayaona na kujifunza moja kwa moja kutoka kwenye TV.Mtu huhisi kuwa anapoteza wakati tu kujistarehesha na TV, anayakata masaa na dakika kwa ajili ya chombo hicho, ni makosa!!.   TV si chombo cha starehe, bali ni chombo kinachotumika kuchochea hisia, kubadilisha muelekeo na utiifu wa mtu. Na ndiyo hali halisi ndugu yangu Muislamu kama bado hujatanabahi.Yafaa Waislamu tuzinduke na kuziona faida chache na hasara nyingi za chombo hiki.  Kama tunaona ni neema hakika tutakuja kuulizwa namna tulivyoitumia.  [At-Takaathur 102:8] ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ - 102:8 Kisha mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa mlizitumiaje. Na kwa hakika hata  masikio na macho tunayoyatumia kwa chombo hicho pia tutakuwa ni wenye kuulizwa. Hivyo ni juu yetu kuchagua ni kipi cha kutizama. [Al-Israa 17:36].  وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا - 17:36 Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa Tv ni kama upanga ukiutumia vizuri unaweza kuleta faida na ukiitumia vibaya unaweza kuleta madhara makubwa.  Kwa mfano mtu akiweza kuidhibiti na kuangalia kwa nadra kwa vipindi vya kheri vyenye kwenda sambamba na dini yetu inaweza kukubalika, bali ni wachache wenye kufanya hivyo.  Wengi wao wameogolea na kuangalia tu bila hata ya kujali faida na hasara zake, na hii ndio iliopelekea madhara kuwa mengi kuliko faida.  Miongoni mwa madhara ya TV ni:- Kunapoteza wakati bure na kupuuza mengi ya wajibu- Inaeneza tamaduni za kikafiri kama ni njia moja ya kuigwa katika maisha- Inaeneza upotofu na uhuru kwa kupitia katika michezo, nyimbo matangazo yasiyo ya heshima ambayo hupelekea watizamaji kutumbuka na tabia hizo za kijinga.- Mazoea ya kuangalia TV yanaharibu akili na kuathiri afya ya mja. Hivyo kama kuna watu wazuri wenye kumuogopa Allah  Subhaanahu Wata’ala na kuonyesha mazuri yenye faida bila ya kukiuka mipaka ya Allah, basi unaweza kuangalia na ni jambo la kupendeza kwa wengi. Ni vyema kuchunga aina gani ya vipindi tunavyoangalia ndani ya majumba yetu.Ni wajibu wa kila mtu kueleweka wazi madhara na faida ya kifaa hichi ili tuweze kukitumia vyema ama kujiepusha nacho kabisa ikiwa tutashindwa kuweka vidhibiti katika majumba jinsi chombo hiki kitumike katika kunufaisha, kuelimisha na kuleta faida na si kuharibu, kupoteza muda na kupelekea jamii iliyozugika na hatimaye kupotoka na kupotosha wengine. Inaendelea IshaAllah.
  • Ummu Nasra  UTANGULIZIHakika shukrani zote ni zake Allaah Subhaanahu Wata’ala, tunaemshukuru, tunaemtegemea, kumtaka msamaha na kutubu kwake. Tunajikinga Kwake Allaah Subhaanahu Wata’ala kutokana na shari za nafsi zetu na makosa ya matendo yake. Mwenye kuongolewa na Allaah hakuna wa kumpotoa, na mwenye kumpotoa hakuna wa kumuongoa. Rehma na Amani ziwe juu ya kipenzi chetu Muhammad SwallaAllahu ‘Alayhi wa Aalihi wa Sallam.‘Amma Ba’ad Nyumba ni neema kubwa ambayo mwanadamu amebarikiwa, وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ - 16:80 Na MwenyeziMungu amekujaalieni majumba yenu yawe maakaazi (yenu) [An-Nahl 16:80] Kuweka mazingira sahihi ndani ya majumba ni jukumu la kila muislam mume na mke, na ni lazima mazingira hayo yaoane sambamba na sheria alizotuwekea Allah Subhanahu wa Ta’ala. Moja kati ya njia ya kuyafikia hayo ni kuepukana na kila aina ya uovu na uharibifu ndani ya majumba. Kuna sababu nyingi kwa mwenye kuamini kuwa makini katika kuijenga na kuilinda nyumba yake katika misingi mema ya kiislam. Miongoni mwa sababu hizo ni: 1. Kujilinda yeye pamoja na familia yake kutokana na moto wa jahannam, na kujiweka mbali na ghadhabu zake. [At-Tahriym 66:6] يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ - 66:6 Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao ambao kuni zake ni watu na mawe 2. Kujua wajibu wake juu ya jukumu la kuchunga nyumba, na kujiweka tayari kujibu kwa kila unachokichunga. Hadith: Kutoka kwa Abdullah, Allah amuwie radhi, kwamba Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Aalihi wa Ssallamamesema: “Nyote ni wachunga na nyote mtaulizwa juu ya mlivyovichunga. Kiongozi anaewaongoza watu ni mchunga na ataulizwa juu wachungwa wake. Mwanamume ni mchunga kwa watu wake wa nyumbani na ataulizwa juu ya wachungwa wake. Na mwanamke ni mchunga kwa nyumba ya mumewe na watoto wake nae ataulizwa juu ya wachungwa wake .Mtumwa ni mchunga katika mali ya bwana wake na anawajibika juu ya mali hiyo. Hakika nyote ni wachunga na na kila mmoja wenu anawajibika juu ya wachungwa wake” Imesimuliwa na Bukhari na Muslim 3. Nyumba ni sehemu ya hifadhi kwa binaadamu, kujiweka mbali na kila aina ya ubaya na uovu ukiwa wa mnyama, binaadamu au majini, na kupata utulivu ndani yake. Amesema Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Ssallam: Usalama wa mtu katika wakati wa fitnah ni kubakia nyumbani kwake. Kilicho muhimu zaidi ni kuzingatia kuwa nyumba ni sehemu nyeti (muhimu) ya kujenga mazingira mazuri ya kiislam, kwani jamii bora hujengeka kuanzia nyumbani. Kwa masikitiko makubwa majumba yetu mengi yamejiweka mbali na mafundisho sahihi ya kiislam. InshaAllaah katika makala hizi tutaweza kugusia na kutanabahisha baadhi ya vitu ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika mfumo wa kiislam ndani ya majumba na jamii kwa ujumla, na kujaribu kutafuta njia muafaka kurejesha mazingira mazuri ndani ya majumba yetu. WabiLlaahi Attawfiyq InshaAllah itaendelea..