Maana Ya Maneno Na Vipengele Muhimu
1. Ameer: Kiongozi msimamizi wa mfuko.
2. Mfuko: Mfuko wa misiba wa Jumuiya ya Al Iman
3. Mchangiaji: Muislamu anaezungumza kiswahili anaetoa michango yake.
4. Mkuu wa familia: Mwenye jukuma la kuisimamia na kuihudumia familia.
5. Mwakilishi: Anaeiwakilisha Jumuiya katika maeneo kusimamia mfuko.
6. Mkusanyaji: Alieteuliwa kukusanya michango wa wanaochangia.
7. Mkurugenzi wa Mazishi: Anaesimamia taratibu za mazishi – Funeral Director.
8. Cheti cha kifo: Death Certificate - cheti kinachotolewa Borough Council kuthibitisha kifo ambacho hukabidhiwa Mkurugenzi wa mazishi.
9 .Ada: Mchango wa Pauni 5.00 kwa mwezi unaotolewa na mchangiaji.
10. Mkaazi: Muislamu anaezungumza Kiswahili anaeishi Northamptonshire.
11. Fomu: Fomu ya misiba inayojazwa na mkuu wa familia.
12. Wategemezi: Wanaomtegemea mkuu wa familia kwa huduma.
13. Mgeni: Muislamu atakaefikia kwa mchangiaji kwa ajili ya matembezi.
14. Akaunti: Akaunti maalum ya mfuko wa misiba.
15 . Stakabadhi: Hati ya malipo (invoice) inayotoka kwa Mkurugenzi wa mazishi.
16 . Notisi: Taarifa ya maandishi kuwapelekea wahusika wa Mfuko.
17. DSS: Idara ya huduma za jamii (Department of Social Services).
18. Direct Debit: Malipo ya moja kwa moja kupitia Benki.( Benki inaweza kumchaji muhusika ikiwa Akaunti haitokuwa na pesa.
19. Standing Order: Malipo ya moja kwa moja kupitia Benki ambayo Benki haimchaji muhusika ikiwa akaunti haitokuwa na pesa.
20. Sadaqah: Ni mchango wa kujitolea kusaidia wasiojiweza.
21. Fomu ya kuridhia; Fomu inayosainiwa na wafiwa kuridhia maiti kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu