Aina ya Mkate Mfano wa Banzi

Vinavyohitajika

Unga wa  ngano  kilo 1

Hamira vijiko  2   vya  kulia  chakula

Chumvi

Ufuta

Siagi ¼  kilo

Samli aina  yoyote  vijiko  2  vya  kulia  chakula

Mayai 5

Maziwa magi 1

Namna  ya  kutayarisha  na  kupika

· Changanya unga kwa kutia maziwa, siagi, mayai, chumvi na  hamira.

· Ili ukandike  vizuri  unaweza  kuongeza  maji. 

· Unga  ukishakandika,  weka  samli  na uukande  kidogo.

· Kata  madonge  kwa  shepu  uipendayo  au  tumia  vibati  vya  kuchomea  mikate.

· Weka  ufuta  juu yake  na  uwache  uumuke  vizuri.

· Choma  kwenye  oven  kwa  gas  mark  5 au  umeme  250

· Baada  ya  dakika  10  itakuwa   tayari  ishawiva, lakini  pia  inategemea nguvu  ya oven.

Kidokezo

· Ni  mizuri  kwa  chai  ya  maziwa  au  ya  rangi (chai kavu)

63 views0 comments

Recent Posts

See All

Biriani ya Kiiran

Vinavyohitajika Mchele vikombe  3 Kuku mgumu  1 Thomu/tangawizi ya  kusaga  vijiko  3 Mdalasini  wa  unga  vijiko  2  vya  chakula Kotmiri kishada  kimoja Mbatata 4 kubwa Zabibu kavu Vitunguu  maji  1

Scones

Vinavyohitajika Cheese (Jibini) 250g Delicate dill (ni aina ya majani ambayo huleta harufu nzuri kwenye chakula kama ilivyo nanaa na kotmiri. angalia kwenye picha) Mayai 5 Unga wa ngano magi 4 Chumvi

Rock Cake

Vinavyohitajika Siagi 250g Sukari 250g Arki rose kijiko 1 cha  chai Zabibu 100g Unga wa ngano 100g Mayai 6 Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Namna ya kutayarisha na kupika Changanya siagi na sukari

Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

Copyrights
Quick Links

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy