Biriani ya Kiiran
Vinavyohitajika
Mchele vikombe 3
Kuku mgumu 1
Thomu/tangawizi ya kusaga vijiko 3
Mdalasini wa unga vijiko 2 vya chakula
Kotmiri kishada kimoja
Mbatata 4 kubwa
Zabibu kavu
Vitunguu maji 10 vikubwa
Bizari nzima vijiko 4 vikubwa (uzile)
Chumvi kiasi
Mafuta ya kupikia
Magi vipande viwili
Namna kutayarisha na kupika
· Teleka kuku na umtie chumvi pamoja na mchanganyiko wa thomu na tangawizi na mdalasini muache awive lakini umbakishe na supu kiasi ya magi 1.
· Chambua majani ya kotmiri uyaoshe na uweke pembeni.
· Kaanga vitunguu maji viwe rangi ya zaafarani (golden brown).
· Menya mbatata na uzikaange ziwe rangi ya zaafarani(zikate vipande vidogo vya kiasi)
Namna ya kutayarisha wali na kuchanganya
· Roweka mchele kwa maji ya baridi kwa dakika 5
· Teleka sufuria ya maji ya wali na utie uzile uchemkie pamoja
· Uzile ukisha toa rangi, utowe kwa kichujio cha chai na weka mchele uchemke mpaka ukiukata uwive kiasi (ukiubinya kwenye mwiko ukatike.
· Uchuje wali maji na tayari kuuchanganya.
· Weka mafuta uliyokaangia vitunguu kwenye sufuria kiasi kijiko 1 cha kula
· Weka wali robo chini ukifuatiwa na kuku na supu yake kiasi.
· Tandaza kotmiri nuru zabibu kiasi na funik a kwa vitunguu vyako ulovikaanga nusu
·Endelea kutia wali wako na kuufuata mfumo huo huo na ukimaliza kwa mbatata na vitunguu
·Malizia kwa kuufunika kwa wali uliobakia na nyunyiza vijiko 3 vya mafuta uliyokaangia vitunguu.
· Funika foil na mfuniko ili mvuke usitoke na uweke kwenye moto mdogo mdogo uwive vizuri kwa dakika 45.
· Ukipendelea kutia kwenye oven pia utawiva vizuri tu.
Kidokezo
Ni wali wenye ladha nzuri na harufu ya kuvutia ukiupatia saladi na ndizi mbivu unapendeza zaidi.
37 views0 comments