Kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Na Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam)

Imetayarishwa na Shani Ahmad


Namshukuru Mwenyezi Mungu, ambae Ametuumba na Akatuweka katika ulimwengu ili tumuabudu Yeye pekee. Na Akatupa miongozo yenye kutuwezesha kuishi katika huu ulimwengu Aliotuumbia. Kisha Akatuletea wajumbe ili watufunze na kutubainishia miongozo hiyo ili tupate kuongoka.


Napenda kuchukua nafasi hii, pia nakuomba na wewe msomaji kuchukua nafasi hii kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), mbashiri wetu na muonyaji wetu.


Kisha ningependa kuanza kwa kusema;


Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipotuumba akatuweka katika huu ulimwengu hakutuwacha tuu, bali alituwekea miongozo ambayo itaweza kutufikisha katika mafanikio ya upeo wa ubora wa maisha duniani.


Akatuletea Mitume ili waje kutufunza na kutuongoza, Akawapa vitabu na sahifa zilizojaa uongofu na rehema Zake.


Ili tupate mafanikio hapa duniani ni lazima tufuate miongozo hii itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tuwafuate Mitume salawatu Llaahi wasalaamuhu ‘alayhim.


Amesema Mwenyezi Mungu:

“Na watahadhari wale wanaopinga amri zake (Mtume) itawapata fitnah au itawapata adhabu iumizayo.” [An-Nuur 24: 63]
Amesema Ibn ‘Uthaymiyn katika Uswuul min ‘Ilmil-Uswuul, ‘kutokana na aya hii tunapata dalili ya kuwajibika twaa ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kwa vile Mwenyezi Mungu Anawahadharisha wale wanaopinga amri za Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa itawapata fitnah ambayo ni misukusuko katika maisha ya dunia au adhabu iumizayo huko Akhera.

Maonyo kama haya hayaji ila kwa kuacha jambo la Wajibu, yaani ni kwamba amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pekee ni Wajibu kuitekeleza’.Endapo mwanaadamu ataacha kumtii Mwenyezi Mungu atakuwa ameacha kutekeleza Wajibu wake, hali ya kuwa amepinga amri ya Mola wake ya kumtii, hali hiyo itampelekea;Kwanza, kuingia katika dhambi ya uasi, ambayo Mwenyezi Mungu Ametuonya kwa adhabu kali ya moto kama Alivyosema katika Surat An-Nisaa:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا - 4:59
“Enyi Mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wale wenye amri miongoni mwenu, na mtakapokhitilafiana juu ya jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa nyinyi ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho…” [An-Nisaa 4: 59]

Aya hii imetuwekea ubainifu kwamba yule ambae hatorudisha khitilafu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume basi huyo si katika Waumini. Hali kadhaalika tunapata mafunzo kama haya katika Surat An-Nisaa:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا - 4:65
“Si hivyo, naapa kwa mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe kuwa ndie hakimu juu ya yale yanayotokea miongoni mwao, kisha wasipate katika nafsi zao kipingamizi juu ya yale uliyohukumu na wajisalimishe kikamilifu.” [An-Nisaa 4: 65]


Haya ni mafunzo kutoka Mola muumba yaliyo wazi yasiyo na shaka, yenye kututhibitishia kuwa twaa ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio mhimili mkuu wa iymaan zetu na Uislam wetu mafunzo haya ni ubainifu ulio dhaahir kuwa bila ya twaa iymaan zetu na kujisalimisha kwetu ni bure na vipi utakuwa Muislam yaani mwenye kujisalimisha ikiwa bado hutekelezi amri za yule unayedai kuwa umejisalimisha kwake?Tatu, kutokufanikiwa katika yale anayokusudia kuyafanya kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu katika Suurat Twaahaa:قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ - 20:123
”Akasema tokeni humo nyote, (kutakuwa na) uadui miongoni mwenu, na ama pale utakapokufikieni kutoka kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu wangu huo, basi huyo hatapotea wala hatotaabika.” [Twaahaa 20 : 123]


Katika aya hii kuna mazingatio makubwa, Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kuwa hata baba yetu Nabii Aadam na mama yetu Hawwaa walipokiuka mipaka yake na kuacha twaa Yake, Aliwatoa katika pepo, pamoja na kuwa walitubu. Aya imeendelea na kutufunza kuwa tutakapokubali kufuata miongozo ya Mwenyezi Mungu hatutopotea wala hatutotaabika.Na mwenye kupuuza amri za Mwenyezi Mungu basi huyo atapata maisha dhiki na taabu hata kama atakuwa na utajiri wa mali na watoto, kwa kutotii amri za Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) mali yake na watoto wake watamtia katika dhiki ameahidi hivyo Mwenyezi Mungu katika Surat Twaahaa kwa kusema:

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ - 3:132
“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.” [Aali ‘Imraan 3: 132]


Katika mafunzo ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni kwamba hatoingia peponi ila yule aliepata Rehma za Mwenyezi Mungu, hivyo tukumbuke kuwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni jambo kubwa mno kwetu, ila kwa yule asie taka pepo katika maisha yake ya Akhera.Na katika kumtii Mwenyezi Mungu tunapata Uongofu kama Alivyosema katika Suuratun Nuur: 54:


“na mkimtii mtaongoka”

Na katika faida za kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kupata utukufu wa kufufuliwa pamoja na watu wema waliohakikishiwa neema za Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, Masadiki, Mashahidi na Maswaalih. Kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Suurat An-Nisaa:

تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ - 4:13
وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ - 4:14


“Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Yeye (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza katika Bustani zipitazo mito mbele yake; wakae humo milele. Na huko ndiko kufaulu kukubwa.”
“na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kuiruka mipaka Yake, (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza Motoni, humo atakaa milele na atapata adhabu zifedheheshazo.” [An-Nisaa 4: 13-14]


Ndugu zangu faida nyingi na hatuwezi kuzidhibiti zote katika makala hii, ni juu yetu kuzijua hivyo tufanye jitihada kuzitafuta ikiwa ni moja ya kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ya kutafuta elimu.Inatupasa tukumbuke kuwa sisi ni Waislam na maana ya kuwa Muislam ni kujisalimisha au kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala), na kuyakubali yale yote aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kama ilivyopokelewa katika vitabu mbali mbali, amesema Abu Ja’afar At-Twahaawiy, katika ‘Aqiidat At-Twahaawiyyah, ‘Aqiydah namba 36,


“Na Uislam wa mtu hautathibiti pasi na kujisalimisha na kujiweka chini ya nguvu za Mwenyezi Mungu...”


Na kujisalimisha maana yake ni kuwa chini ya twaa ya Mwenyezi Mungu, kufanya kila Alilotuamrisha na kuwacha kila Alilotukataza, kumkusudia yeye tu katika ibada na mambo yetu yote ya maisha yetu.Ikiwa hatuwezi kuitimiza ahadi hii adhimu tuliyompa Mwenyezi Mungu ya kujisalimisha Kwake au kuwa tayari kutekeleza maamrisho Yake yote na kuyakubali yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) wapi tunashika katika kujivunia Uislam wetu?
Maana Ya Sunnah


Ni ufahamu wa wengi miongoni mwetu kuwa Sunnah ni vitendo au ibada ambazo tunapozitekeleza tunapata ujira, na tunapo yawacha hatutopata adhabu bali tutakosa ujira tu.


Kutokana na ufahamu huu watu wengi wamejengeka na tabia ya kutotekeleza Sunnah na kusema ‘hiyo ni Sunnah tu si wajibu’, pale wanapotakiwa kutekeleza amri kati ya maamrisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).Kwa hakika Sunnah ni mafundisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), ikiwa ni miongoni mwa maneno, vitendo au yale yaliyofanywa mbele yake nae akayakiri.


Na juu ya haya ndipo tunalazimika kutekeleza Sunnah katika hali ya kuwajibika juu yetu kama ilivyobainishwa katika aya zilizokwisha tangulia hapo juu. Aya ambazo zinatuhimiza kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).


Hali hiyo ya kuwajibika kwetu katika Sunnah inaondoka pale tu Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) anapotubainishia, au kubainishwa na wanavyuoni kwa kufuata taratibu zake zinazokubalika.


Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Fiqh


Kwanza kabisa tufahamu kuwa Sunnah ni neno la Kiarabu lenye maana ya njia ‘mwenendo’ yaani ni jambo ambalo limetokea kisha watu wakafuata mwenendo au jambo hilo. Kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam):

“Mwenye kuweka mwenendo mzuri basi atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakaofuata mwenendo huo, na mwenye kuweka mwenendo mbaya atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakao fuata mwenendo huo...”

Hii ni maana ya Sunnah katika lugha.


Ama katika matumizi ya Sunnah kwa wataalamu wa Fiqh, ni amali zilizo chini ya Waajib, zinakusanya kila kile ambacho Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekipendekeza ambacho hakiwajibiki kukifanya.


Sunnah kwa mtazamo huu hujulikana kama Manduub (mapendekezo) na hupata ujira mwenye kuzitekeleza na hatoingia makosani yule mwenye kuziacha. (M. H. Kamali, Hadith Studies)


Na huu ndio mtazamo ambao wengi wetu tunaufahamu, mtazamo wa ki- Fiqh ambao umelenga katika kutoa hukumu za kishari’ah, na si maisha ya Wanaadamu ya kila siku kwa ujumla.


Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Hadiyth


Vivile katika historia ya Dini, neno Sunnah limetumika kwa namna kadha, kwa mfano Wanachuoni wa Ahlul-Hadiyth, wanaitambua Sunnah ni chochote kile kilicho thubutu kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Semi zake , Matendo yake, Yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia, historia yake, Tabia na Maumbile yake. Baadhi ya Maulamaa wamewaita Wanachuoni wa Hadiyth ndio Ahlu-Sunnah.


Baadhi ya Wanachuoni wakubwa wa karne ya tatu Hijriyyah waliandika vitabu kuhusiana na ‘Aqiydah na kuyapa majina As-Sunnah. Zama hizo watu walikuwa wanajulikana ni watu wa Sunnah kama ni katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah. Pia ilitumika kinyume cha Sunnah; Bid'ah (Uzushi) kwa kubainisha wale ambao si katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah.


Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Uswuuliyyuun


Amma Wanachuoni wa Uswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika.


serifUswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika.15 views0 comments

Recent Posts

See All

BAADHI YA DUAA NA ADHKAAR MUHIMU

KUNUIA HAJJ NA UMRA Labbayka Allahumma Umra Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Umra Labbayka Allahumma Hajj Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Hajj TALBIYAH Labbayka-Llaahumma labbayk labbayka laa s

Yenye Kuhatarisha Nyumba za Waislamu - 3

Ummu Nasra 2.  MUZIKI NA NYIMBO Miongoni mwa yenye kuzoeleka katika majumba yetu ni mziki.  Kwa kweli mziki umeenea kila pembe ya dunia kiasi ambacho unawaumiza Waislamu wengi kimwili na kiakili bila

Yenye Kuhatarisha Nyumba za Waislamu - 2

Ummu Nasra Kuna mambo mengi ya wazi kabisa ambayo sheria yameyakataza katika Uislamu na jamii imeghafilika nayo.  Mambo hayo huchangia  kuharibika na kuhatarisha mfumo  mzima wa kiislam ndani ya majum

Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

Copyrights
Quick Links

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy