Makaroni Ya Kubeki

Vinavyohitajika

Makaroni ½ kilo

Kuku au nyama ¼ kilo

Tangawizi na thomu(iliyosagwa-paste) kijiko1 cha chakula

Pilipili manga iliyosagwa ½ kijiko cha chakula

Ndimu 1

Chumvi

Unga wa  mahindi (fine corn flour) vijiko 3 vya chakula

Mozarella cheese ½ kilo

Tungule(Tomato/Nyanya) 3

Kitungu maji 1

Mafuta ya kupikia vijiko 2

Tungule ya kibati kijiko 1 cha chakula (tomato puree)

Pili pili ya unga kiasi

Namna Ya Kutayarisha  Na  Kupika

· Mkate kuku vipande vidogo vidogo na umuoshe vizuri.

· Mchemshe  kwa  thomu, tangawizi, chumvi na ndimu pamoja pilipili manga na ya unga ili apate kukolea vizuri  na kisha umuweke  pembeni.

· Weka  maji  magi moja kwenye sufuria na kisha utie chumvi na pilipili manga kidogo na unga wa mahindi na uanze kupika uji wa gravy na hakikisha  usiwe mwepesi sana na uwe mzito wa kiasi.

· Katakata kitunguu na umenye tungule (nyanya/tomato) ukaange mchuzi lakini bila ya kuunguza vitunguu na umalizie kwa kutia chumvi na nyanya puree. Pia hakikisha mchuzi huu usiwe na maji mengi ninachokusudia uwe dikodiko.

· Yachemshe  makaroni  mpaka yawive  vizuri.

· Weka makaroni kwenye tray ya kuchomea kwa kuyapanga makaroni nusu kwanza na kuweka kuku kidogo kisha mchuzi pamoja na gravy kwa kumalizikia na cheese.

· Endelea kufanya mfumo huo kwa juu yake tena na tayari kwa kuyachoma kwenye oven gas mark 8.

· Yafunike Makaroni kwenye foil kwa dakika 10 ili cheese iyayuke na baadae yafunue na kuyaacha kwa dakika 5 ili uipate rangi nzuri ya wekundu mwanana.

Kidokezo

Unaweza kuongeza mboga mboga uzipendazo ili kukifanya chakula kiwe na afya na lishe zaidi.

25 views0 comments

Recent Posts

See All

Biriani ya Kiiran

Vinavyohitajika Mchele vikombe  3 Kuku mgumu  1 Thomu/tangawizi ya  kusaga  vijiko  3 Mdalasini  wa  unga  vijiko  2  vya  chakula Kotmiri kishada  kimoja Mbatata 4 kubwa Zabibu kavu Vitunguu  maji  1

Scones

Vinavyohitajika Cheese (Jibini) 250g Delicate dill (ni aina ya majani ambayo huleta harufu nzuri kwenye chakula kama ilivyo nanaa na kotmiri. angalia kwenye picha) Mayai 5 Unga wa ngano magi 4 Chumvi

Rock Cake

Vinavyohitajika Siagi 250g Sukari 250g Arki rose kijiko 1 cha  chai Zabibu 100g Unga wa ngano 100g Mayai 6 Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Namna ya kutayarisha na kupika Changanya siagi na sukari

Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

Copyrights
Quick Links

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy