Mboga ya Kabichi
Vinavyohitajika
Kebichi (Cabbage) 1
Kitunguu maji 1
Mbatata 2 za kiasi
Tungule 2(nyanya)
Bilingani 1
Pilipili mboga 1
Carrot 2
Chumvi
Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya kulia chakula
Bizari ya manjano
Bamia vidole 7 (ukipenda)
Namna ya kutayarisha na kupika
· Likate kebichi na uliweke pembeni.
· Zimenye mbatata na uzikaange pamoja na bilingani, bamia na uziweke pembeni(unapokaanga visiwe vyekundu sana)
· Injika sufuria na uweke mafuta kiasi na ukaange kitunguu maji
· Kabla hakijawa chekungu weka bizari, koroga kiasi ya sekunde 5 na katia tungule huku ukikoroga.
· Koroga kidogo na uweke mboga ya kebichi pamoja na carrot, pilipili mboga ambazo utakuwa umezikata kata.
· Punguza moto na uwache mboga iwive kwa mvuke.
· Baada ya dakika 5 changanya mbatata na bilingani na uwache ikauke ila isiwe na maji mengi
Kidokezo
Mboga hii ina afya sana kwa sababu unaipika kwa mvuke pia unaweza kuongezea mboga mboga nyengine ili uipambe zaidi kwa afya bora.
Usisahau kuweka chumvi
62 views0 comments