Mkate wa Chila
Vinavyohitajika
Mchele magi 2
Nazi ya cream ½ au ya kibati 1
Hamira kijiko 1 ½ cha kulia chakula
Hiliki iliyosagwa ¼ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Maji ya vuguvugu magi 1 ikiwa utatumia nazi ya maji ya kibati na magi 2 ikiwa utatumia nazi ya kipande (cream coconut)
Sukari ¼ kikombe cha chai
Mafuta kidogo ikiwa yatahitajika wakati wa kuchoma chila
Namna ya kutayarisha
· Roweka mchele kwenye maji kwa masaa kumi.
· Saga mchele kwa kutumia blender na uchanganye vitu vyote nilivyoviorodhesha hapo juu isipokuwa ute wa yai tu.
· Hakikisha vimesagika vizuri (mchele usiwe na chenga nyingi).
· Weka ute wa yai na usage tena kidogo tu.
· Uwache unga uumke.
Namna ya kupika
· Tumia chuma kisichogandisha (non stick).
· Chota mchanganyiko kwa upawa au kijiko chenye uvungu wa kiasi cha chuma utachotumia kuchomea.
· Injika chuma ili kipate moto na uweke kijiko kimoja cha upawa na ufunike mpaka iwive vizuri au (ikauke)
· Itowe uiweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa ikiwa unapenda kula vitu vya moto na ikiwa laa isubiri ipowe
Kidokezo
Kuwa makini kwa kutumia moto mdogomdogo kwa kuchomea chila kwa kuhofia zisiunguwe na juu zikawa mbichi (Ili kuipata chila laini na mwanana lazima unga uwe laini na usiwe mzito kama wa vitumbua au mkate wa mchele).
78 views0 comments