MUKHTASARI WA HUKUMU ZA JANAAZAH


Imekusanywa na Shani Ahmad

Bismillahir Rahmaanir Rahiym

AlhamdulilLlaah, was swalaatu wa salaam ‘alaa Muhammadin (Salla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Anapokuwa Katika Hali Ya Kutoka Roho

· Wanaohudhuria mauti ya Muislam wanatakiwa wamlakinie Shahadah.

Yanapobainika Mauti Yake

· Kumfumba macho.

· Kulainisha viungo vyake ikibidi.

· Kumvua nguo zake.

· Kumuweka kitandani.

· Kumuombea Du’aa.


 • Kumfunika.

 • Kuanza matayarisho ya maziko.

Yanayojuzu Kwa Wanaohudhuria

 • Kumfunua uso na kumbusu.

 • Kulia pasina kunung’unika na kuomboleza au kuchupa mipaka.

Yanayowapasa Watu Wa Karibu Ya Maiti Pindi Wanapopata Habari Za Kufiliwa

Kusubiri na kuridhia Qadhaa ya Mwenyezi Mungu na asome du’aa hii:


“Hakika sote tunatoka kwa Allaah, na Kwake sote tutarejea, Nakuomba Allaah unipe ujira katika msiba wangu huu na unifidie na kilicho bora zaidi.”

Yaliyoharamishwa

 • An-Niyaahah nako ni kuomboleza kwa kunung’unika na kupiga kelele (kunaongeza huzuni na kuondosha subira, na kujikubalisha na Qadhaa ya Allaah).

 • Kuchana nguo.

 • Kunyoa nywele.

Kukosha Maiti

 • Hukumu yake ni Fardhi Kifaayah.

 • Siqtwi (kilichoanguka; kiumbe kilichoharibika tumboni kwa mama yake) huoshwa ikiwa ni baada ya miezi minne.

 • Shahidi wa uwanja wa mapambano haoshwi hata akiwa na Janaba

 • Si fardhi kuosha maiti ya kafiri, bali inajuzu kwa Muislam kumousha jamaa yake akiwa miongoni mwa makafiri.

 • Walio bora kuosha maiti ni familia yake.

 • Inajuzu mume kumuosha mke na kinyume chake.

 • Anapofariki mwanamke miongoni mwa wanaume, na mwanamme miongoni mwa wanawake, na pakakosekana muoshaji wa jinsia ile. Kwa hali kama hiyo inapotokea, maiti hutayamamishwa. Wanaume watamtayamamisha mwanamke na Wanawake watamtayamamisha mwanamme hali ya kuwa maiti yupo na nguo zake.

Sifa Za Muoshaji

 • Muoshaji kuwa na sifa njema na usiri.

 • Kuwa na elimu ya kuosha

Faida: inajuzu mwenye hedhi au mwenye janaba kuosha maiti kwa vile hakuna dalili inayokataza.

Namna Ya Kukosha Maiti

 • Huoshwa mara tatu au tano au saba…

 • Kwa maji na majani ya mkunazi (sabuni), na josho la mwisho lichanganywe na kaafuur.

 • Mwanamke afumuliwe nywele zake. Zisukwe tena mikia mitatu baada ya kuoshwa na kutupwa nyuma yake na si kifuani kwake.

 • Kuwepo na upole na huruma

 • Muoshaji anaanza kwa kumchua tumbo kwa upole kutoa uchafu ulio baki.

 • Kumtawadhisha Wudhuu wa Swalah.

 • kumuosha kichwa na shingo pamoja na ndevu.

 • Amuoshe upande wa kulia kuanzia shingoni mpaka kwenye kisigino na upande wa nyuma.

 • Upande wa kushoto kama alivyofanya upande wa kulia.

 • Atakaushwa maji.

 • Yatakapokosekana maji atatayamamishwa.

 • Atakapozikwa bila ya kukoshwa atafukuliwa endapo hajaharibika.

Faida: Mwenye hedhi au janaba huoshwa josho moja tu kwa vile hukumu za kishari’ah hazimuwajibikii tena. Na mwenye kukosha maiti haimuwajibikii kukoga; akipenda ataoga, akipenda atanawa mikono yake.

Kumkafini

 • Kumkafini maiti ni Fardhi Kifaayah.

 • Kafani inunuliwe kutokana na mali ya maiti.

 • Inajuzu kujinunulia kafani kabla ya mauti.

Sifa Ya Kafani

 • Ya mwanamme (na hata ya mwanamke) ni shuka tatu.

 • Inapendeza ziwe nyeupe.

 • Inapendeza ziwe za pamba.

 • Iwe safi na yenye kusitiri.

 • Itiwe manukato.

 • Mwenye kuhirimia mashuka mawili na asifunikwe kichwa.

 • Shahidi kafani yake ni nguo zake alizofia nazo.

 • Ya mwanamke ni kama ya mwanamme. Imezoeleka mwanamke vipande vitano vya nguo lakini Hadiyth inayofundisha hivyo si sahihi, hivyo ni bora kushikamana na mafunzo sahihi yanayoonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya mwanamme na mwanamke katika kafani japokuwa kuna baadhi ya Wanazuoni wamependekeza hivyo.

Baada Ya Maziko

 • Kulipa madeni yake haraka.

 • Kutoa pole (taazia) kwa kusema:

"Hakika ni cha Allaah Alichokichukua na ni Chake Alichokitoa, na kila kitu mbele Yake kina muda maalum, hivyo subiri na utaraji malipo.”

Haya ndio tuliyojaaliwa kutoa katika Sunnah na Allaah Ndie Mjuzi zaidi.

37 views0 comments

Recent Posts

See All

BAADHI YA DUAA NA ADHKAAR MUHIMU

KUNUIA HAJJ NA UMRA Labbayka Allahumma Umra Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Umra Labbayka Allahumma Hajj Nimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Hajj TALBIYAH Labbayka-Llaahumma labbayk labbayka laa s

Yenye Kuhatarisha Nyumba za Waislamu - 3

Ummu Nasra 2.  MUZIKI NA NYIMBO Miongoni mwa yenye kuzoeleka katika majumba yetu ni mziki.  Kwa kweli mziki umeenea kila pembe ya dunia kiasi ambacho unawaumiza Waislamu wengi kimwili na kiakili bila

Yenye Kuhatarisha Nyumba za Waislamu - 2

Ummu Nasra Kuna mambo mengi ya wazi kabisa ambayo sheria yameyakataza katika Uislamu na jamii imeghafilika nayo.  Mambo hayo huchangia  kuharibika na kuhatarisha mfumo  mzima wa kiislam ndani ya majum

Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

Copyrights
Quick Links

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy