Rock Cake
Vinavyohitajika
Siagi 250g
Sukari 250g
Arki rose kijiko 1 cha chai
Zabibu 100g
Unga wa ngano 100g
Mayai 6
Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula
Namna ya kutayarisha na kupika
Changanya siagi na sukari mpaka ichanganyike vizuri.
Weka mayai kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari.
Tia arki.
Changanya unga na baking powder.
Utie unga kwenye mchanganyiko wa mayai, siagi sukari kidogo kidogo mpaka uone haukushiki mikononi.
Ipake siagi au mafuta sahani ya kuokea - tray na uzipange rock cake.
Zichome kwa gas mark 5 mpaka ziwe na wekundu wa kupendeza.
Kidokezo
Jitahidi zisikauke na zikaungua sana zitakuwa ngumu na kila zikikaa zinazidi kuwa nzuri.
20 views0 comments