Scones

Vinavyohitajika

Cheese (Jibini) 250g

Delicate dill (ni aina ya majani ambayo huleta harufu nzuri kwenye chakula kama ilivyo nanaa na kotmiri. angalia kwenye picha)

Mayai 5

Unga wa ngano magi 4

Chumvi

Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula

Single cream au double cream 300ml

Siagi 250g

Namna ya kutayarisha na kupika

Changanya unga, siagi na baking powder pamoja na chumvi.

Kata kata delicate dill uchanganye kwenye unga.

Ikate Jibini kwenye chombo cha kukatia - Grater na kisha itie kwenye unga.

Yachanganye mayai na  cream  uyachape  vizuri.  

Anza kumimina mchanganyiko wa cream na mayai kwenye mchanganyiko wa unga.

Utapata mchanganyiko uliokuwa  laini  lakini  unaweza  kusukumika. 

Weka  unga  mkavu  kwenye  kibao  cha  kukatia  usukume  na  kata  shepu  uipendayo.

Zipange kwenye tray ya kuchomea.

Paka yai juu ya scones.

Zichome  kwa  muda  wa  dakika  25 to 30 kwa  gas  mark 5.

Zikiwiva ziache  zipoe  na  tayari  kwa  kuliwa.

Kidokezo

Scones  unaweza  kuzifanya kwa  shepu uipendayo, hasa  watoto  ni chakula wanachokipenda na  ni  kizuri  kwa  afya  yao  kwa  sababu  ya jibini.

Pia kwa  kupata  rangi  nzuri  ya kupendeza  paka yai  lilochanganywa   na double  au single  cream

11 views0 comments

Recent Posts

See All

Biriani ya Kiiran

Vinavyohitajika Mchele vikombe  3 Kuku mgumu  1 Thomu/tangawizi ya  kusaga  vijiko  3 Mdalasini  wa  unga  vijiko  2  vya  chakula Kotmiri kishada  kimoja Mbatata 4 kubwa Zabibu kavu Vitunguu  maji  1

Rock Cake

Vinavyohitajika Siagi 250g Sukari 250g Arki rose kijiko 1 cha  chai Zabibu 100g Unga wa ngano 100g Mayai 6 Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Namna ya kutayarisha na kupika Changanya siagi na sukari

Aina ya Mkate Mfano wa Banzi

Vinavyohitajika Unga wa  ngano  kilo 1 Hamira vijiko  2   vya  kulia  chakula Chumvi Ufuta Siagi ¼  kilo Samli aina  yoyote  vijiko  2  vya  kulia  chakula Mayai 5 Maziwa magi 1 Namna  ya  kutayarisha

Al-Iman Society of Northamptonshire

Society of Northamptonshire, Based in Northampton Mosque and Islamic Centre, 72 Clare St, NN1 3JA

Email: info@al-iman.co.uk

Phone: 07961 284919

Registered Charity: 1117020

Copyrights
Quick Links

© 2018 by Al-Iman - All materials are Copyrights to Al-iman  |  Terms of Use  |   Privacy Policy