Vipapatiro vya Kuchoma
Vinavyohitajika
Vipapatiro vya kuku (wings) robo kilo.Chumvi.Pilipili manga kijiko1 cha chai.Bizari nzima iliyosagwa kijiko1 cha chai.Paprika vijiko 2 vya chakula.Tangawizi na thomu iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula.Ndimu moja nzima kubwa na yenye maji ya kutosha.Mdalasini uliosagwa kijiko 1 cha chai.
Namna ya kutayarisha na kupika
Visafishe vizuri vipapatiro na kisha vioshe. Viweke kwenye bakuli la kuwachanganyia huku umevigida maji vizuri.Weka viungo vyote kwa pamoja uvichanganye vizuri. Vikishachanganyika, vikamulie maji ya ndimu na uvichanganye tena vizuri.Vitie kwenye baking tray na uvichome kwenye grill huku ukivigeuza geuza mpaka viwive na viwe na rangi ya hudhurungi.Weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Kidokezo
Ukiwa mpenzi wa pilipili utaongeza, pia unaweza kuvitia maziwa ya kuganda(mtindi) vijiko vinne vya chakula wanazidi ladha nzuri zaidi.