Wali wa Zabibu
Vinavyohitajika
Mchele 1 kg
Vitunguu maji 1kg
Mbatata 4 kubwa
Thomu na tangawizi iliyosagwa vijiko viwili vya kulia chakula
Kuku mmoja au nyama kilo moja
Zabibu kavu ¼ kg
Bizari nzima unga vijiko 2 vya chakula
Mdalasini wa unga vijiko 2 vya chakula
Chumvi
Mafuta ya kupikia
Magi ya chakula (kijani /zaafarani)
Namna ya kutayarisha na kupika
Chemsha kitoweo kwa thomu na tangawizi, bizari nzima na mdalasini.
Kikishawiva weka pembeni (bakisha supu kiasi).
Menya vitunguu maji uvikate na uvikaange mpaka viwe na rangi nzuri ya wekundu.
Zimenye mbatata na uzikaange pia mpaka ziwe nyekundu
Roweka mchele kwa muda wa dakika 10 (lakini inategemea mchele unaotumia, mchele huu ni basmati)
Teleka maji ya kupikia wali na weka chumvi kiasi
Subiri maji yachemke na kisha weka mchele.
Uwache uchemke mpaka ukiuvunja kwa kidole uwe unagawanyika.
Umwage maji.
Weka mafuta uliyokaangia vitunguu vijiko viwili vya chakula kwenye sufuria.
a.Weka wali kiasi
b.Weka kuku na supu, vitunguu, mbatata na zabibu
Fuata mfumo huo kwenye awamu mbili ya wali na mwisho nyunyiza mafuta kiasi ya robo kikombe cha chai na pia ni wakati wa kuzitia rangi kwenye sehemu tafauti.
Funika foil na mfuniko juu ya wali na uweke moto mdogo kwa muda wa dakika 45
Ufunuwe na uuchanganye vizuri uupakuwe na tayari kwa kuliwa
61 views0 comments