Home
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 1
Thursday, 01 March 2012 20:29

 

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Kila sifa jema inamstahikia Allaah Aliyetukuka Muumba wa ulimwengu na walimwengu wake, Swalah na Salamu zimfikie kipenzi cha Waislamu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Sahaba zake kiraam (Radhiya Allaahu 'anhum) na kila anaewafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho.

Shari’ah, amri, makatazo na kanuni ni katika taratibu ambazo jamii haiwezi kiziepuka ikitaka kuwa na uadilifu, amani, usalama na uhuru kwa wana jamii wake. Jamii ni mchanganyiko wa wema, wabaya na kadhalika; hivyo huhitaji utaratibu wa kuwadhibiti, kuwazuia au kurekebisha na kuwatengeneza wale wenye kwenda kinyume na shari’ah ziliopo katika jamii ile; kwa kuwawekea adhabu, faini, fidia na kadhalika; lakini walio wema –raia wema- na wenye kufuata kanuni huwa hawana chao kitu, kwani hawawekewi –tunzo- kwa kufuata au kutunza kwao kanuni zaidi ya kuongezewa ushuru.

Uislamu ni mfumo kamili wa maisha kwa jamii, mfumo wenye kujitegemea usiohitaji mchango wa aina yo yote ile kutoka pahala popote pale katika jambo lolote lile; mfumo huo umekuja na mengi yakiwemo maamrisho na makatazo; shari’ah na kanuni; adhabu na malipo mazuri yasiyobagua baina ya kiongozi na mwenye kuongozwa; mfalme na raia; sharifu na dhaifu; tajiri na maskini; mweusi na mweupe, mwanamke na mwanamume na kadhalika; Qur-aan inasema:

“Na anayefanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini; basi hao wataingia Jannah wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende” [An-Nisaa 4: 124]; kwa lengo la kuhakikisha kuwa wote wananufaika katika maisha yao ya duniani; na kwa wale Waumini wa Allaah na Siku ya Qiyaamah kutarajia malipo mema kutoka kwa Mola wao kwa kule kutekeleza kwao Amri Zake na kujikataza na Makatazo Yake bila ya kuendekeza au kufuata matamanio ya nafsi zao; kwa kuelewa na kuwa na yakini kuwa iymaan yao haikamili bila ya kumtii Mola wao na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Amri Zake na kujikatza na Makatazo Yake tena bila ya kuwa na khiari au uchaguzi katika Aliyoyahukumu kama isemavo Qur-aan:

“Haiwi kwa Muumini wa kiume wala Muumini wa kike Anapohukumu Allaah na Mjumbe Wake jambo wakawa wanakhiari –yakuchagua kinyume cha Alivyohukumu Allaah- katika jambo……” [Al-Ahzaab 33: 36].

Maamrisho na makatazo hayo yamekuja katika Qur-aan tukufu na katika Sunnah sahihi za Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); maamrisho au makatazo hayo huja na kumlenga mkusudiwa awe mwenye hadhi au cheo cha aina yoyote ile na adhabu yake haibagui kwa wenye kwenda kinyume na maamrisho awe sharifu au dhaifu; tajiri au maskini na kadhalika, kwani huko –kubagua kwa kuwaadhibi baadhi na kutokuwadhibu wengine- ni kuangamia kwa jamii kama tunavyoona katika ulimwengu wetu na kama alivyobainisha (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kusema:

Last Updated on Thursday, 01 March 2012 20:59
Read more...
 
MWONGOZO KATIKA KUJIANDAA NA MAISHA YA NDOA
Thursday, 01 March 2012 19:59

 


Imetayarishwa na: Abu-Ammaar

UTANGULIZI

Shukurani zote ni kwa Allah Subhaanahu Wata’ala aliyetakasika na aliyetukuka. Rehma na amani zimfikie Mjumbe wake Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam aliyeletwa kwetu ili iwe ni rahma kwa walimwengu wote.

Unapokaribia wakati wa kutaka kuoa/kuolewa, mume/mke mtarajiwa hutingwa na masuala mengi vipi aanze kutafuta mchumba, sifa gani achague katika kumpata mshirika wake wa maisha na vigezo gani atumie katika kufikia lengo lake.

Masuala haya huwatinga watarajiwa na huku wakiwa na mitazamo tofauti katika machaguo yao na mazoeya, desturi na tamaduni yakichangiya kwa kiasi kikubwa katika kuathirika huko. Watarajiwa wengine hawafahamu wanahitaji wake/waume wa aina gani, hivyo wanajikuta kama wanaoingiya sokoni bila kujua wanataka kununua nini hasa.

Na jengine ni baadhi ya watarajiwa kujiingiza katika chuo cha ndoa bila ya kupata taaluma yoyote inayohusiana na maisha hayo na hatimaye kukosa uwezo wa kuziendesha ndoa zao.

Hata hivyo maandalizi haya huwa yanafanyika kwa kiasi kikubwa katika idara nyenginezo na kwa ufanisi mkubwa ila tu katika suala la kimsingi la dini, maandalizi haya huwa hayana nafasi wala kupewa kipaumbele na mara nyingi huwa ni suala la mwisho linaloangaliwa kwa baadhi (likibahatika).

Last Updated on Thursday, 01 March 2012 20:05
Read more...
 
« StartPrev12345678NextEnd »

Page 1 of 8

Who's Online

We have 3 guests online

Administrator

Wahusika